Maisha yanaenda kasi sana. Vitu vinatokea ila hatuwezi kuzuia siku zisiendelee na maisha yasichukue nafasi yake! Basi hebu tuzungumzie muziki wetu kidogo hasa upande wa wasanii wa kike;

Hili wazo lilinijia punde nilipoona nomination za tuzo za Afrimma, kategori ya wasanii bora wa kike wa Afrika Mashariki - Jina la Maua Sama likaniijia kichwani.

Kusema kweli, unapoongelea wasanii wa kike bora kuwahi kutokea kwenye muziki wa Bongo Fleva huwezi ukaacha kulitaja jina la Maua Sama hata kwa bahati mbaya. Na ukiacha kulitaja basi ni wazi hauujui muziki au ni chuki binafsi tu.

Embu tuwe wakweli. Ni nani ambaye hafahamu sauti nzuri na tamu ya huyu dada?? Sauti ambayo haichoshi wala haikeri kusikiliza awe anaimba kusifia au hata awe anaimba kulalamika ni lazima utapenda.

Upangiliaji wake mzuri wa mashairi na kadhalika kwenye muziki wake tutakubaliana kuwa anajua!! Kama nakumbuka vyema hajawahi kutembelea kiki ukitoa matatizo madogo madogo ambayo kila binaadamu anayo!! Kwa kifupi Maua anajua. Ni mmoja kati ya wale watu ambao ukiwapa ndimu ukidhani kuwa unawakomoa, utarudi ukute wameikamua na kutengeneza sharubati ya 'lemonade' wanakunywa zao taratibu bila hata shida. Teh Teh Teh!... Mwenye sifa mpe sifa zake bwana.

Lakini pamoja na hayo yote kuna jambo ambalo naona haliko sawa... Mara ya mwisho nasikia sauti ya Maua ikipita juu ya mdundo ilikuwa ni kwenye wimbo ALIYOSHIRIKISHWA na Darasa - Jina la wimbo ni Tumepoteza. Nimeandika neno 'aliyoshirikishwa' kwa herufi kubwa hapo kabla nikiwa na maana ya kuwa toka mwaka 2019 umeanza mpaka sasa Maua hajatoa wimbo wake kama msanii solo. Kwanini?? Sijui ndio maana nauliza.

If I remember right, wimbo wake wa mwisho ni IOKOTE ambao ulitoka mwaka jana. Bonge moja la hit song - Wimbo wa taifa in other words.! Umetengeneza zaidi ya 13M views upande wa video na zaidi ya 2M views upande wa audio on YouTube! Jambo ambalo hata Vanessa, one of the female artist held in high esteem in Bongo Fleva, hajalifanya kwenye career yake mpaka sekunde hii ninapoandika huu uzi.

Kwa hio fact niliyotaja hapo juu, like most of you, mimi nilitegemea kuona back to back. Wimbo baada ya wimbo. Show kila ikitoka show na vitu kibao kutoka kwa Maua. To my surprise, Picha na Caption za IG throughout the year ndio zimezidi.

Thing is kuna watu wanampenda Maua alafu kuna sisi tunampenda Maua na kazi zake. Kukaa kimya ni kutunyima haki yetu... Watu wake wa karibu, Fadhili Kondo, kama bado wewe ni meneja hebu fanya kitu.

Maua pia. Kama utaiona hii elewa we knew you from your music and we want it to stay that way! Do both us a favor, Tupe muziki na sisi tutakupa the love you deserve.

Naomba tutafsiri kimya chako kama KISHINDO KIKUBWA. Hebu ione hii thread halafu upate haja ya kutupa muziki. We love you!! And we intend to keep it that way. Please.

JF