Mkali wa Muziki wa BongoFleva kwa sasa Omary Ally 'Marioo', amesema hawezi kutoka kimapenzi na msanii mwenzake Amber Lulu, kwa kile alichokidai msanii huyo ana mambo mengi sana ambayo yeye hayawezi.


Marioo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI cha East Africa Television, kinachoruka kila Jumatano kuanzia saa 8:30 mchana.

Marioo amesema kuwa "mimi sina mpenzi kwa sasa, niko single hizo habari za Amber Lulu si za kweli, kwanza ana mambo mengi kuliko mimi, anasafiri sana na anafanya mambo mengi sana pia ni mkubwa."

Aidha Marioo amesema moja ya vigezo vyake ambavyo lazima mwanamke anayetoka naye kimapenzi, asiwe na wafuasi zaidi ya 6000 katika mtandao wa Instagram.

"Mimi napenda mwanamke wangu awe mzuri, lakini asiwe na mambo mengi asiwe anapenda sana umaarufu, mwanamke akiwa na 'followers' zaidi ya 6,000 Instagram huyo siwezi kuwa naye."