Zimbabawe imeleza kutofurahishwa pakubwa kwa hatua ya Marekani kumuekea vikwazo Anselem Nhamo Sanyatwe, balozi wake nchini Tanzania.

Katika taarifa ya hivi punde, serikali ya Harare hiyo imeitaja hatua hiyo ya Marekani kama inayodunisha uhuru wa taifa hilo na ambayo 'inashinikiza migawanyiko badala ya kuidhinisha uponyaji wa taifa na maelewano'.

Wizara ya mambo ya nje Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya Balozi Sanyatwe, ambaye ni Brigedia mstaafu ya jeshi la kitaifa la ulinzi wa rais, kutokana na "kuhusika kwake katika ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu."

Wizara hiyo Marekani imefafanua kuwa ina taarifa za kuaminika kwamba Anselem Sanyatwe alihusika katika msako mkali dhidi ya raia Zimbabwe ambao walikuwa hawakujihami wakati wa ghasia zilizozuka mnamo Agosti mosi mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu, uliosababisha vifo vya raia wasita.

Ghasia zazuka nchini Zimbabwe
Jeshi la Zimbabwe 'liliwatesa waandamanaji'
Zimbabwe imesema inapokea kwa uzito hatua ya 'baadhi ya mataifa yenye nguvu' yaliojichukulia hatua binfasi kuidhinisha hatua ambayo 'ni wazi zipo nje ya mtazamo na barua ya tume iliyoidhinishwa Zimbabwe kuchunguza ghasia hizo za baada ya uchaguzi.