Mario Balotelli ameweka wazi kuwa mama yake alilia alipomwambia kuwa amerudi kuichezea klabu ya Brescia iliyopo katika mji aliyokulia nchini Italia.

Hata hivyo Balotelli baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru na kurudi kucheza Serie A kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu, Balotelli amemthibitisha  kuwa hana hofu ya kushindwa ku-perform Italia kama ilivyokuwa kwa AC Milana na kurudi England.Balotelli alizaliwa Palermo na kuhamia katika mji wa Brescia akiwa na umri wa miaka 2 na bado familia yake iliyomuasili (adopt) ina ishi Brescia japokuwa baba yake alishafariki toka 2015.

“Mama yangu alilia nilipomwambia kuwa nafikiria kwenda kujiunga na Brescia, alikuwa na furaha sana, sina hofu hata kidogo ya kushindwa kufanya vizuri, nipo sawa na mtulivu”>>> Balotelli

Inaaminika kuwa Balotelli ambaye mara ya mwisho hakufanya vizuri katika Ligi ya Italia na kukumbwa na majeruhi amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo iliyopanda daraja baada ya kukataa ofa ya kujiunga na klabu ya Flamengo ya Brazil.