Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, hakika inasikikitisha kwa tukio la mwanamama kukiri kumuua mkwe wake, Dmitry Bogdanov (32) ambaye alikuwa mume zamani wa binti yake kwa kumkata korodani zake. Tukio hilo limetokea nchini Urusi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni pesa anazodaiwa na binti yake baada ya talaka yao.


Baada ya tukio hilo, binti aliamua kuwapigia simu polisi baada ya mama yake kumjulisha kuwa kile alichotenda. Kijana huyo alifariki baada ya kukatwa mara 27 mfululizo na mkwe wake.
Polisi wamedai mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 49 alitenda kosa hilo katika eneo la la Novgorod huko Urusi ambapo ni nyumbani kwake, na baada ya kutenda unyama huo alitupa viungo hivyo dirishani.

 Eneo walilokuwa wakipatia kinywaji washitakiwa na marehemu kabla ya mauaji (Picha na East2West News)
Mauti yalimfika kijana huyo baada ya kujumuika na kupata kinywaji na mama mkwe pamoja na mume wa mama mkwe, lakini katikati ya maongezi mama mkwe alimlaumu bwana Bogdanov kwa kushindwa kumpatia fedha binti yake ambaye ni mke wake wa zamani kwaajili ya matunzo ya mwanae waliyezaa na binti yake hadi kufikia yeye kujitolea kumhudumia bintiye. Baada ya malumbano hayo mama huyo alikasirika na kuchukua kisu na kuanza kutenda unyama huo.

 Kijana huyo alifariki baada kuchomwa na kukatwa mara 27 kwenye korodani na mama huyo. Baadae mume wa mama huyo alichukua kisu na yeye kuendelea kumchomachoma. Chanzo cha Polisi kilieleza

Baada ya kumaliza kufanya unyama huo, mama huyo alimpigia simu bintiye na kumueleza mkasa mzima na baadae bintiye akaamua kuwapigia simu pilisi na kuwapa taarifa. Baada ya mama huyo na bwana’ake kukamatwa na polisi walikana kufanya tukio hilo lakini hatimaye baadae walikubali kuwa walimuua kijana Bogdanov. Chanzo cha Polisi kilidaiKamati ya Uchunguzi nchi Urusi (Russian Investigative Committee) wamefungua jalada la mashtaka kuhusiana na tukio hilo.