Rais wa Manzese Madee 'Seneda' amefunguka kuhusu sakata la kuvunjika kwa ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya.


Madee ameeleza hayo kwenye kipindi cha "FNL'' ya East Africa Television, baada ya kuulizwa alikuwa upande gani baada ya kuvunjika kwa ndoa hiyo,

"Wale ni watu maarufu lakini linapokuja suala la mahusiano yao nawachukulia kama watoto wangu na marafiki zangu, vitu vingi ambavyo tunaviongea nyuma ya pazia siwezi kuviongea hapa, sidhani kama nitakuwa sahihi, yale ni mahusiano yao, waliamua kuanza na kuyamaliza wenyewe"

Aidha amejibu tuhuma za kutupiwa lawama kuhusu kuvunjika kwa mahusiano ya Dogo Janja na Irene Uwoya ambapo amesema, watakuwa wanamuonea kwa sababu hawezi kumshika Dogo Janja, kumpangia wala kumzuia mwanamke wa kutongoza.

Pia ameendelea kusema kuwa alishirikishwa katika kuanzisha mahusiano yao hadi yalipovunjika pia alishirikishwa na wote alikuwa anaongea nao vizuri tu.