Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amewataka mabalozi wa Tanzania kushirikiana na shirika hilo ili kuweza kuleta maendeleo ya mradi inayoendelea hapa nchini na pia kulitangaza taifa kwa ujumla.
Akizungumza na Mabalozi hao waliotembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge(SGR) unaendelea, Kadogosa amesema kuwa mpaka sasa ujenzi umefika asilimia 60.4 hivyo amewashukuru mabalozi waliokuja kuangalia mradi wa kimkakati kwani kutawawezesha kulitangaza taifa kwa mazuri yanayoendelea.
“Kama tunaweza kutekeleza miradi hii kwa pesa yetu, watu wa nje wanatuheshimu kwahiyo uwekezaji mkubwa kama huu unawagusa wawekezaji wa nje kwahiyo sisi tunawashukuru mabalozi kuja kuangalia miradi hii hivyo watakaporudi huko watawaelezea watu wa huko miradi hii walioyoiona kwa ukubwa wake,”amesema Kadogosa.
Aidha, Kadogosa amesema kuwa gharama za kutengeneza fensi katika ujenzi wa reli hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ni dola bilioni 1.2 kujumlisha na kodi na kutoka Morogoro kwenda Maktupola Singida ni dola bilioni 1.9 pamoja na kodi hivyo jumla ya gharama zitakazotumika ni takribani bilioni 3.1.
Naye Balozi wa Tanzania nchini Swedeni, Wilibrod Slaa amewataka watanzania waweze kujivunia kumpata Rais mwenye kufanya maamuzi kwani wameona miradi mingi ikifanyika hapa nchini kwani hata nchi zilizoendelea wamekuwa wakifanya uwekezaji na ulipaji kodi ambazo zinasaidia kuibua miradi mbalimbali