DAR ES SALAAM: Kumekucha tena! Baada ya ukimya mrefu kupita tangu apate msala wa kutekwa na watu wasiojulikana, mkali wa michano ya Hip Hop, Bongo, Ibrahim Musa ‘Roma’ amekwaa skendo nyingine; safari hii anasakwa na polisi kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Mtoa taarifa makini  ameeleza kuwa, msanii huyo amekwaa tuhuma hizo mwaka 2016 lakini amekuwa akichengachenga kulipa hali ambayo imemfanya jamaa aliyempa fedha hizo kuamua kulivalia njunga suala hilo. “Iko hivi, kuna jamaa anaitwa

taarifa huyo alidai kuwa Roma aliingia mitini baada ya kuona Diamond amepewa malazi mazuri katika Hoteli ya Ngonga wakati yeye (Roma) akitakiwa kulala katika hoteli ya kawaida. “Yaani aliona kama ameshushwa thamani akaamua kusepa zake jambo ambalo lilimkera muandaaji wa shoo hiyo,” alisema. Amani lilimvutia waya Ezekiel ambapo alipopatikana alithibitisha maelezo ya mtoa

taarifa na kusema amechoshwa na ahadi za uongo za Roma hivyo mwaka huu atahakikisha anamsaka popote alipo kwa sababu ameshamfungulia mashtaka polisi. “Nina RB yake na polisi wanaendelea kumsaka, naona ananifanya mimi mpumbavu lakini anatakiwa kutambua jasho la mtu haliwezi kwenda bure,” alisema na kumuonesha mwanahabari wetu jalada la mashtaka lililosomeka MAG/RB/2735/2019 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU.

Alipotafutwa Roma kwa nyakati tofauti kuhusu suala hilo simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi, licha ya kuonesha umemfikia na kuusoma lakini hakujibu chochote.

Ezekiel Clement, alikuwa anaandaa matamasha siku za nyuma, sasa Roma alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliotakiwa kwenda kupafomu katika Hoteli ya Ngonga Kyela, Mbeya lakini dakika za mwisho aliingia mitini. “Ezekiel aliendelea na shoo hiyo bila uwepo wa Roma kwani alikuwepo pia Diamond (Nasibu Abdul) ambaye alikamua na mshabiki wakaridhika,” alisema mtoa taarifa huyo. Akizidi kushusha ubuyu, mtoa

GPL