ULIKUWA ukijiuliza zile nguo zote za mwigizaji Wema Isaac Sepetu alizokuwa akizivaa alipokuwa bonge ziko wapi? Taarifa ikufikie kuwa, kumbe baada ya kuona zinamvaa, aliona isiwe taabu, akazipeleka kwenye kituo cha watoto yatima.



Wema ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, cha kwanza kabisa alipoona mwili wake umepungua, alizipeleka nguo kwa mama yake kisha wakashauriana kuzipunguza kidogo na kuwapelekea watoto yatima.


“Hakuna hata nguo moja iliyokuwa inanikaa tena maana zote zilikuwa kubwa kupitiliza hivyo nilipunguza nyingine nikapeleka kwa watoto yatima na nyingine nitajua nitazifanyeje baadaye,” alisema Wema ambaye siku hadi siku anapungua.