Korea Kaskazini imeiba dola bilioni mbili (£1.6bn) kufadhili mpango wake wa silaha kupitia uvamizi wa kimtando, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja.

Ripoti hiyo ya kisiri inasema Pyongyang inalenga mabenki na na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-currency kukusanya pesa.

Vyanzo vya habari vimethibitishia BBC kwamba UN ilikuwa ikichunguza mashambulio 35 ya kimtandoa.

 Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un amesema hatua hiyo ni onyo dhidi ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini.

Pyongyang imeelezea kuwa mazoezi hayo yanakiuka mkataba wa amani.


How could war with North Korea unfold?
Ripoti t iliyovuja na ambayo ilitumwa kwa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini katika Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, inasema Pyongyang "ilitumia uhalifu wa hali ya juu wa kimtandao kuiba pesa kutoka kwa taasisi za kifedha na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-kukusanya mapato yake".

Wataalamu pia wanachunguza shughuli za kimtandao zinolenga malipo kupitia fedha za kigeni.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa shambulio la Korea Kaskazini dhidi ya sarafu ya crypto- imeisaidia "kukusanya fedha kwa njia ambazo ni vigumu kutambuliwa na ikilinganishwa na ukaguzi wa kawaida unaofanywa na sekta ya benki".