Kisa Baba Yake Alitupa Gari Mtoni
Kijana mmoja nchini India aliyejulikana kwa jina la Akash mwenye miaka 22, ametupa gari ya kutembelea aina ya BMW katika mto wa Haryana uliopo kaskazini mwa nchi hiyo.


Gari hilo lenye thamani ya Sh 128 milioni, alinunuliwa kama zawadi na baba yake mzazi kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.

Akash ameeleza sababu ya kufanya hivyo kuwa ni kutolipenda gari hilo ambalo thamani ya yake ni bei ya chini huku yeye alikuwa anataka gari la aina ya Jaguar lenye thamani ya Sh. milioni 193.

Aidha wakati analitupa gari hilo alikuwa anarekodi video ambayo imesambaa katika mitandao ya kijamii ndani na nje ya India ikimuonyesha akifanya tukio hilo.

Polisi wamesema kijana huyo aligundulika kuwa ana matatizo ya akili na alionekana amekosa furaha baada kununuliwa gari la aina hiyo na Baba yake.