WINGA wa zamani wa Simba, Shiza Kichuya ameweka wazi kwamba baada ya muda wake kumalizika ndani ya klabu ya ENNPI ya Misri kwa sasa anatamani kuondoka nchini humo huku akiwa tayari kurejea Tanzania.Kichuya aliondoka Simba, Februari mwaka huu na kujiunga na ENNPI ambayo aliichezea kwa mkopo ambapo kwa sasa amerejea Tanzania mara baada ya muda wake wa mkataba kumalizika.Winga huyo amesema kwa sasa malengo yake ni kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupata changamoto mpya ambapo kama akikosa anaweza kurejea Tanzania kwa ajili ya kujipanga zaidi.

“Ninaweza nikarudi au nikaenda sehemu nyingine, lakini maono yangu ni kwenda sehemu nyingine juu zaidi ya pale nilipokuwa. Hayo ndiyo malengo yangu ambayo nimejiwekea kwa sasa.“Ninaweza kubadilisha timu au kubakia hapo ENNPI, kuangalia changamoto zaidi baada ya kukaa nao. Lakini katika suala la kurudi hapa kucheza hakuna kisichowezekana katika maisha ya soka kwa kuwa na hapa kuna timu bora, ninaweza kurudi kwa ajili ya kujipanga zaidi ili baadaye niende tena mbele,” alisema winga huyo. Baadhi ya timu kubwa hapa Tanzania ni Simba ambayo alitoka, Yanga na Azam FC.