Nahodha wa Argentina Lionel Messi amezuiwa amepigwa marufuku kucheza mechi za kimataifa kwa muda wa miezi mitatu baada ya kudai kuwa shirikisho la soka la Amerika Kusini -Copa America ni “fisadi”. Mshambuliaji huyo wa Barcelona , mwenye umri wa miaka 32, alikatazwa kucheza wakati Argentina iliposhinda 2-1 na kuwa katika nafasi ya tatu ilipoishinda Chilena baadae akasema ” kombe lilipangwa kwa ajili ya Brazili”.



Pia amepigwa faini ya dola 50,000 (£41,121) na Conmebol, shirikisho la mpira wa miguu la Amerika Kusini.

Messi ana siku saba za kukata rufaa juu ya uamuzi wa Conmebol wa kumzuwia kucheza mechi.

Marufuku ina maanisha Messi atakosa mechi zijazo za kirafiki za Argentina dhidi ya Chile, Mexico na Ujerumani Septemba na OctobaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Marufuku ina maanisha Messi atakosa mechi zijazo za kirafiki za Argentina dhidi ya Chile, Mexico na Ujerumani Septemba na Octoba
Marufuku hiyo ina maanisha Messi atakosa mechi zijazo za kirafiki za Argentina dhidi ya Chile, Mexico na Ujerumani Septemba na Octoba.

Mechi ya kufuzu ya Argentina kwa ajili ya kombe la dunia la mwaka 2022 inaanza Machi 2020.

Kufuatia kushindwa 2-0 kwa Argentina katika nusu fainali na wenyeji Brazil, Shirikisho la soka la Argentina lililalamika juu “makosa mabaya na makubwa ya waamuzi “.

Katika kujibu malalamiko hayo , shirikisho la Conmebol lilisema shutuma za kuhoji maadili ya Copa America “hazina msingi” na “zinaonyesha ukosefu wa heshima “.

Messi alionyeshwa kadi nyekundu katika kipindi cha dakika 37 za mechi dhidi ya Chile, kufuatia makabiliano na Gary Medel, ambaye pia alifukuzwa uwanjani.

“Hatupaswi kuwa sehemu ya ufisadi huu,” alisema Messi . “wametuonesha ukosefu wa heshimakatika kipindichote cha shindano hili.

“La kusikitisha, ufisadi, na waamuzi, hawataki kuwaruhusu watu kufurahia soka, wanaiharibu kidogo .”