Baada ya siku kadhaa kuripotiwa kuwa mwimbaji Katy Perry amekutwa na hatia ya wizi wa hatimiliki kupitia wimbo wa ‘Dark Horse’ ulioachiwa rasmi 2013 na kuelezwa kuwa wimbo huo ni copyright kutoka kwa ‘Joyful Noise’ ulioimbwa na mwimbaji wa Injili Flame.

Sasa leo August 2,2019 kupitia matando wa ‘The New York Times’ umeripoti kuwa kampuni ya Capitol Records pamoja na Katy Perry watalipa fidia ya kiasi cha thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 6 za Kitanzania ambapo Mahakama imeamuru kuwa Katy atalipa shilingi Bilioni 1 na pesa nyingine zilizobaki zitalipwa na kampuni hiyo ya muziki ya Capitol kwa mmiliki halali wa ngoma hiyo ambae ni Marcus Gray ‘Flame’.

Hata hivyo Jumatatu ya July 29,2019 iliripotiwa kuwa Mahakama ya mjini New York iliwakuta na hatia watu sita akiwemo muandaaji wa nyimbo (prouducer), mtunzi wa nyimbo Sarah Hudson na Juicy J.