UKIACHANA na mechi tatu za kirafiki ambazo kipa mpya wa Simba, Beno Kakolanya ameitumikia timu hiyo, jana mara ya kwanza aliiongoza katika Ligi ya Mabingwa Afrika huko nchini Msumbiji dhidi ya UD Songo.Kabla ya mchezo wa jana, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems aliliambia Spoti Xtra kuwa; “Kakolanya anafanya vizuri, sina wasiwasi tena kama ilivyokuwa msimu uliopita pindi Manula alipokuwa
akiumia.”“Katika mechi zote alizocheza amefanya vizuri kwa hiyo ni matumaini yangu kuwa kadiri siku zinavyoenda atakuwa bora zaidi na atatoa changamoto kubwa Manula kuhakikisha anakuwa bora zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita,” alisema Aussems.