Msanii mkongwe wa filamu Blandina Chagula maarufu kama Johari amefunguka kuhusu kashfa za wasanii wa Bongo Movie kuiba wake na waume za watu.

Johari amepiga stori na EATV&EA Radio Digital kuhusu kuhusu kashfa hizo ambapo amesema kuwa,

"Hapana mimi sidhani kama ni Bongo Movie peke yake, nahisi hawajafanya tafiti vizuri, wakifanya utafiti vizuri zaidi sehemu zozote hata watu wanaokaa maofisini hivi vitu vipo, sehemu yoyote yenye mkusanyiko wa watu mbalimbali na rika tofauti haya mambo yanatokea kwa sababu kila mtu anatabia zake".

Johari ameendelea kusema kuwa  sifa hizo wanasemwa wasanii wa Bongo Movie kwa sababu kwao yanaonekana zaidi, ila hata watu wengine wanafanya mambo makubwa tu.

Pia msanii huyo amezungumzia siri ya urembo wake na kuonekana mpya kila siku wakati amekuwa kwenye tasnia kwa muda mrefu.

"Siri ni kujitunza tu, mwili ni kama gari la mkaa ukilipeleka sana safari nyingi linakuwa linachoka, nafanya mazoezi kidogo na sijichoshi sana katika mapenzi pia mapenzi hayana nafasi katika maisha yangu" amesema Johari.