WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ametoa wiki mbili kwa halmashauri zote zilizokusanya mapato chini ya asilimia 50 ya malengo yao kuandika barua ya kujieleza kwa Katibu Mkuu TAMISEMI ya kwanini wasichukuliwe hatua kwa kutofikia malengo.
Pia amesema Wakurugenzi walioshindwa kukusanya mapato watapewa vinyago vya uzembe na kutofikia lengo kisha kutakiwa kuviweka mbele ya ofisi zao na za wakuu wa mikoa hiyo.
“Vinyago nitakavyovitoa vitakuwa na sura mbaya sana na Wakurugenzi wa halmashauri hizo wanatakiwa kuviweka kwenye ofisi zao na ofisi za wakuu wa mikoa husika,” amesema.
Waziri Jafo amezitaja halmashauri tano zilizoongoza kwa kigezo cha wingi wa mapato yaliyokusanywa (pato ghafi), Jiji la Dodoma limeongoza kwa kukusanya sh. bilioni 71.7, Halmashauri za Manispaa za Ilala sh. bilioni 58.2, Kinondoni (Sh.Bilioni 34.0), Temeke (Sh. Bilioni 33.3) na Ubungo (Sh. Bilioni 18.6). .
“Mikoa iliyoongoza ni Dar es Salaam (Sh. Bilioni 163.6), Dodoma (Sh. Bilioni 82.7), Mwanza (Sh. Bilioni 32.7), Arusha (Sh. Bilioni 31.9) na Mbeya (Sh. Bilioni 31.4)” amesema Jafo.
Ameitaja mikoa mitano ya mwisho kwa kigezo cha wingi wa mapato yaliyokusanywa (pato ghafi) ni Njombe (Sh. Bilioni 11.5), Simiyu (Sh. Bilioni 8.8), Rukwa (Sh. Bilioni 8.2), Kigoma (Sh. Bilioni 7.8) na Katavi (Sh. Bilion