Image result for shachihataKAMPUNI moja nchini Japan  imetengeneza kifaa maalum cha kuwatambua wanyanyasaji (wapapasaji) wa kingono katika magari ya usafiri wa umma.

Kampuni ya kiteknolojia inayofahamika kama Hachihata ya Japan imetengeneza kifaa hicho ili kukabiliana na uhalifu wa kingono ambacho kitamfahamisha muathiriwa kujua kama kuna mtu anampapasa na kitamweka alama ya wino ambayo haionekani kwa mhalifu.

Kampuni hiyo imesema kuwa  iliamua kutengeneza kifaa hicho ili kuwadhibiti watu wanaowanyanyasa kingono abiria katika vituo vya treni ila inahofia kifaa hicho kinaweza kutumiwa vibaya na watu wenye chuki dhidi ya watu fulani.

Pia ilitangaza wazo la kubuni kifaa hicho kwa mara ya kwanza mwezi wa tano baada ya video moja kusambaa mtandaoni inayowaonesha wasichana wawili wa Japan wakimkimbiza mhalifu wa unyanyasaji wa kingono katika kituo cha usafiri wa treni .