Mwanaume mmoja amekamatwa jijini Madrid akishukiwa kuchukua video za uchi za wanawake zaidi ya 550 kinyume cha sheria.

Mwanaume huyo ana miaka 53 na ana asili ya Colombia, amerekodi video kupitia simu yake ya mkononi aliyoificha kwenye begi lake la mgongoni.

Polisi wamesema kuwa alizirusha mtandaoni video 283 katika tovuti za ngono na zikapata mamilioni ya watazamaji.

Wengi wa walengwa wa video hizo, baadhi ni wadogo chini ya umri wa miaka 18, walilengwa maeneo ya usafiri wa treni.

Wazazi wanaouza video za ngono za watoto mtandaoni
Vijana 1000 washtakiwa kutumia Facebook kueneza video za ngono
Daktari apatikana na video ya watu wakishiriki ngono na nyoka
Mwanaume huyo anashukiwa kuchukua video hizo tangu mwaka jana ambapo alianza kuziweka katika mitandao.

Alikua akirekodi pia katika maeneo kama masoko ya kisasa, kuna wakati alikua akijitambulisha kwa walengwa wake ili aweze kupata video nzuri.

Polisi walianza kumfatilia na kumkamata akirekodi mwanamke mmoja kwenye treni.