Baba mmoja aitwaye Saidu Dan Iya raia wa Nigeria amemkata koo mwanaye wa kike aitwaye Zahra Saidu mwenye umri wa miaka 8.


Baba huyo ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya kisaikolojia baada ya kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu, ambapo inadaiwa alimkaba mwanaye shingoni kisha kumkata koo kwa kutumia kisu.

Mama mzazi wa mtoto huyo Fadimatu Saidu ameeleza kuwa alipigiwa simu na jirani yake jana mchana baada ya kutokea kwa tukio hilo.

“Mimi ni mfanyakazi za ndani katika familia ya watu, Niliondoka asubuhi na kumuacha mwanangu akiwa amerudi kutoka shule akiwa na baba yake, lakini baadaye nilipigiwa simu na jirani yangu nirudi nyumbani ili kujionea tukio hili la jaribio la mauaji kwa mwanangu”, amesema mama wa mtoto huyo.

Baba huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi na anashtakiwa kwa makosa mawili ya kihalifu ambayo ni kushambulia kwa kutumia silaha na kutoa vitisho vya kuuwa kwa mke wake.

Mtoto kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini na Daktari amesema kuna asilimia 50 za kupona au kupoteza maisha ila watatoa matibabu bila ya gharama zozote.