Majina yake halisi ni Jacqueline Wolper Masawe a.k.a @wolperstylish . Alizaliwa tarehe 18.12.1987 huko Moshi Mkoani Kilimanjaro. Ni muigizaji, Mwanamitindo,mjasiriamali na muongoza filamu Tanzania, alipata elimu ya msingi Magrath Primary School na baadae alijiunga na elimu ya sekondari Ekenywa Secondart school na mwisho alijiunga na chuo cha ICC kujifunza lugha na masomo mengine ya biashara

Ameshiriki kwenye Filamu mbalimbali kama Kipenzi Changu, Surprise, Red Valentine, Family Tears, Ndoa yangu na nyinginezo nyingi tu. Alishawahi kushinda tunzo ya Ijumaa Sexiest Girl mnamo mwaka 2012

Kwenye swala la mahusiano hayupo nyuma, alishatajwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mastaa mbalimbali kama @officialalikiba ambaye ndiye alikuwa mpenzi wake wa kwanza (Mfungua dimba) toka aanze kujihusisha na mambo ya kimahusiano, @juma_jux @diamondplatnumz , @harmonize na kuna tetesi kuwa kwasasa bwana mdogo muuwaji kutoka Jiji lenye miamba mingi Tanzania ndio anamiliki kibubu cha furaha cha mrembo huyo

Kwasasa Jacqueline Wolper anamiliki kampuni yake ya mitindo inayofahamika kwa jina la #HouseOfStylish inayohusika na ubunifu wa mavazi mbalimbali. Kampuni hii inamfanya Jacqueline Wolper kuwa kati ya mastaa wakike wenye mkwanja mrefu Tanzania. Ndoto yake kubwa ni kuja kuwavalisha mastaa wakubwa duniani kama #Rihanna na wengine wengi