Hatimaye meneja wa msanii nyota wa Bongo Fleva Diamond ambaye pia ni moja ya viongozi wa Lebo ya Muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB), Sallam SK amekata mzizi wa fitna baada kuthibitisha kuwa msanii Harmonize ameandika barua ya kuvunja mkataba na lebo hiyo.

Akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Block 89 kinachoruka kupitia redio ya Wasafi FM, Sallam amesema kwa sasa wanasubiria kufanya taratibu za kisheria kuuvunja mkataba na soon watakuwa na kikao cha kukubaliana terms ingawa Harmonize ameshaonyesha nia ya kukubaliana na terms zote za kuterminate mkataba.“Harminize kwa sasa hivi ndani ya moyo wake hayupo WCB, Harmonize kimakaratasi bado yuko WCB. Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya ku-termnate (kuvunja) mkataba wake na yuko willing (tayari) kupitia vipengele vya mkataba wake,” amesema Sallam.

Amesema wao kama uongozi wamevutiwa na ustaarabu wake kwani msanii huyo ameamua kufuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kukutana na viongozi wote wa WCB kwaajili ya mazungumzo rasmi.Amesema hawawezi kumzuia msanii yeyote kuondoka WCB kama anaona kuna maslahi makubwa zaidi akifanya kazi nje ya taasisi hiyo na watampa ushirikiano wote ikiwa kama ameondoka kwa ustaarabu bila mkwaruzano.

Ni takribani mwezi mmoja umepita tangu taarifa za Harmonize kutaka kujiondoa WCB kuibuka kutokana na msanii huyo kuondoa neno ‘signed under WCB’ kwenye sehemu ya bio yake ya Instagram na kuweka WCB4LIFE.Suala lingine lililoibua mjadala ni juu ya msanii huyo kum-follow msanii nyota wa Bongo Fleva Ali Kiba ambaye ni hasimu na mpinzani mkubwa wa Diamond Platnumz ambaye ndiyo bosi wa WCB.

Hata hivyo, si uongozi wa Harmonize mwenyewe au uongozi wa WCB ambapo ambao ulitoa ufafanuzi juu ya jambo hio na kuendelea kuzua sintofahamu kwa mashabiki wa wasanii wa taasisi hiyo mpaka jana Sallam alipovunja ukimya.

Sallam ameomba radhi kwa mwenendo uliokuwa ukioneshwa na msanii huyo siku za karibuni na kuwaasa mashabiki wa Wasafi kuendelea kutoa sapoti kwa Harmonize kwani hajaondoka kwa ubaya.

Maoni ya wadau mbalimbali na mashabiki

princeiddy_97
Wcb wanyonyaji yaani upige show ya ml50 yako 15 nyingine za diamondπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ bado rayvan mtabaki na queen darleen tu

ramakalamba
Waswahili bhana mna mambo ya ajabu sana,,,, et tumkatae ndani ya mwaka mmoja chini,,,, sasa akiwa chini ww utafaidika na kitu gani? Mmekalia roho mbaya tu ndio maana mnaishia kuwa maskini maisha yenu yote 😈😈😈

angelonelson9763
Aondoke tu tumemjua kupitia mondi aondoke tu.

kendrickplatnumz4
#Unfollowharmo

dogo__la__diamond
Nilitaka kujua ukwel leo nimeupataa

tizoarsenal
Kwanzia leo tumkataeee mwanaaaa miaka miwili tu chali πŸ€”πŸ€”πŸ€”

albaone2909
Ni kama mtoto kumwambia babaake nataka kwenda kujitegemea…#hakuna tatizo ila mashabiki maandazi ndo wanatokwa mapovu wakati huenda ndan ya familia wenyewe wako poa tuu. #WASAFI wampe baraka zote na waendelee kutengeneza kina harmonize wengine na Mungu atawazidishia.

luogajr13
Tunasubr kauli tu tumkatae mwana

simba_wa_morogoro
Mseng Mfupi Anajikuta Kama Mmbuu

elly03_official
Hajui WCB ni maji asepe tu mm nta mblock πŸ˜‚

queen_of_mashauzi
Bora nilishamuunfollow Mudaa akwendree salamaaa

vumbi_la_kongo_mbeya
Mwacheni aondoke km moyo wake haupo WCB mnabak nae wa kazi gan? Asije kuwahrbia brand yenu buree..πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ

official_jaysontz
Doh hata Yesu alikaa na kufanya miujiza mingi na wanafunzi wake lakini mwishowe alipata msaliti haikotosha wote wakakimbia 😒😒 ila dhambi ya kuwa msaliti ni kali sana mark my word guys

kapingageorge7777
Aendeee tuuu ila akae akijua kwambaa hatokuwa harmo yule wa WCB bado hana ukubwa huo wa kutoka WCB amuulize Mavokoo yuko wapi tangu katoka WCB hajulikani kama ni underground au ni star

abdullatifu_juma
vipi kuhusu uwanja anaotaka kujenga Daimondi nikweli au

abdulimkama
Dah bac ndo kapotea kama akitoka hapo mmmh amuulize rich mavoco hahahah kaka harmo umepotea mmmh

njombicomediani
Hta akisepa aina xhidaaa watakuja na wengne ye nan?bna

twahirmjeda8
mimi tayari nisha unfollow na unsubscribe page zote

offsetrick
Kweli wendio umesema @

john_the_trending
Be blessed harmo I know wale wenye four watakupinga but naelewa we ni mtu wa namna gan

ngalemba_ngelebwike
Nyie wapiga dili wanyonyaji, wabinafsi munaua kundi tatzo sio diamond tatzo nyny mameneja kumamake zenu asa ww

eliah.john.16
Wamemuweza mavoko tu uyo dgo hamumwezi hata kidgo mnazani uyo baraka da prince