Msanii wa muziki wa Hip Hop Dudubaya aka Mamba Konk Konk Konk Master Oil Chafu leo hii Jumapili ya August 25,2019 ameokoka na kufanyiwa ibada ya maombi na Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' wa Kanisa la Inuka Uangaze lililopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo maarufu nchini Tanzania Godfrey Tumaini, maarufu kwa jina la kisanii kama Dudu Baya, Leo Jumapili ametangaza kuokoka rasmi na kujiunga na kanisa la Boniface Mwamposa.

Godfrey Tumaini ametangaza hilo leo hii Jumapili tarehe 25 August 2019 katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe.