Meneja wa kundi la Wasafi,  Sallam amesema msanii Harmonize  kwa sasa ndani ya moyo wake hayuko WCB, isipokuwa tu yupo kimakaratasi na tayari ameshaandika barua ya komba  kuvunja mkataba na kundi hilo.

Akizungumza na Wasafi TV, Sallam amesema hata katika tamasha la Wasafi lililofanyika mjini Mwanza, Harmonize alitumia usafiri binafs na  kufanya baadhi ya mambo yaliyotoa tafsiri kuwa ameshajitenga na WCB.

“Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.

“Sisi katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize” amesema Sallam na kuongeza;

“Harmonize ameshatuma barua ya maombi Wasafi kuvunja mkataba wake na yupo tayari kufuata sheria zote.

“Sisi tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali.