Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara na wenzake watatu wameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Haji Manara
Imeelezwa kuwa wanadaiwa deni na fidia ya Tsh. milioni 83.3 baada ya kupokea bidhaa zenye nembo ya Dela Boss Perfume bila kuzilipia.

Mbali na fedha hizo, Mlalamikaji aliyejitambulisha kwa majina ya Abu Masoud Al Jahdhamy, Ameiomba mahakama kuwaamuru washtakiwa hao watatu ambao ni, Haji Manara, Beatrice Ndungu na Palm General Supply kumlipa fidia nyingine itakayoona zinafaa ikiwemo gharama za mawakili.

Kesi hiyo ya madai yenye namba 128/2019 ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mwandamizi, Wanjah Hamza, Imeahirishwa mpaka tarehe 29 Agosti Mwaka huu itakapotajwa tena.

Katika madai ya msingi, mlalamikaji amefungua kesi hiyo akiwadai walalamikiwa fedha hizo baada ya kuwasambazia bidhaa zenye nembo ya “De La Boss Perfume” Tanzania na bidhaa hizo zimetengenezwa Dubai.