Msanii kutoka kundi la Weusi G Nako Warawara, ameeleza sababu zinazomfanya asiitoe picha ya aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.G Nako Warawara ameiweka picha hiyo ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye 'Profile Picture' ya mtandao wa kijamii wa Instagram.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, msanii huyo ameeleza sababu za kutotoa picha hiyo.

"Kwa sababu namkubali tu yule mzee na napenda awepo pale nafikiri ni mtu ambaye nimetokea kumuelewa na nimeshawahi kukutana naye mara mbili au mara tatu nikatokea kumuelewa na nafikiri anastahili kuwepo pale na napenda aendelee kukaa pale hadi nitakapoamua".

Picha hiyo ya Gnako akiwa na Dkt. Jakaya Kikwete imekaa kwa muda zaidi ya miaka mitatu, ikimuonyesha staa huyo wa muziki akiwa ameshikana mkono na aliyekuwa Rais huyo mstaafu.

Pia msanii huyo amezungumzia suala lake la kupenda kusaidia wasanii chipukizi.

"Mimi naamini  hapa duniani sipo milele nipo kwa muda tu, wakati mwingine kutokana na roho yangu jinsi ilivyo naonaga huruma kuona wasanii chipukizi wakilala studio ndio maana nikiona mtu mwenye kipaji namsaidia", amesema Gnako Warawara.