FC Barcelona wametia nia sasa wanawashawishi Coutinho na Rakitic wampate Neymar
Club ya FC Barcelona ya Hispania tayari imeripotiwa kuwa imeanza mazungumzo rasmi na club ya Paris Germain ya Ufaransa kwa ajili ya kumrudisha Neymar katika himaya ya Nou Camp.

Mtandao wa ESP umeripoti kuwa Barcelona wametenga dau la euro milioni 100 pamoja na kuwashawishi Philippe Coutinho na Ivan Rakitic wakubali kujiunga na PSG kama sehemu ya usajili wa Neymar.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Neymar aliwahi kuichezea FC Barcelona kwa misimu minne (2013-2017) kabla ya kushinikiza kuhama timu hiyo na kwenda kujiunga na PSG na sasa yupo mbioni kurudi.