Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia afya Dk. Doroth Gwajima,akizungumza na watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akiwaonyesha kadi ya CHF iliyoboreshwa wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia afya Dk. Doroth Gwajima, amewataka watumishi wa afya kote nchini kuacha kuwabagua au kutowapa kipaumbele wateja wanaotumia kadi za bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa kuwahudumia watu wenye fedha mkononi kwanza.

Dk. Gwajima ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa wilayani hapo.

Amewataka watumishi wa afya kuwapa kipaumbele wagonjwa wanaotumia kadi hizo ili kuweza kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo nchini.Dk Gwajima Amewataka watumishi kote nchini kuendelea kuhamasisha matumizi ya kadi hizo ili kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo hapa nchini na watu wengi waweze kujiunga.Amesema hivi sasa kadi za CHF iliyoboreshwa imefanyiwa marekebisho makubwa na serikali hali ambayo inamwezesha mgonjwa kupata huduma katika hospitali yoyote hadi ngazi ya mkoa.

Pia amewataka watumishi wa afya nchini kutoa huduma zenye ubora ili kuweza kuwavutia wananchi kujiunga na mifumo hiyo ya bima ya afya ya jamii.“Kama tusipotoa huduma bora hivi vituo vyetu tulivyojenga nchi nzima vitakuwa havina maana lazima sisi kama watumishi wa afya tubadilike ili kuweza kuwavutia wananchi kuja katika vituo vyetu kupata huduma ya afya”

“Sitaki kusikia baada ya siku hizi 14 kuwa kuna kituo kimeshindwa kutuma taarifa zake au mifumo inakataa kwani kila kituo kinatakiwa kutuma taarifa zake za wateja waliohudumiwa ili kuweza kurejeshewa fedha zake ambazo zitatumika katika mahitaji mbalimbali ya eneo hilo”amesema Dkt Gwajima.

Naye mganga mfawidhi wa kituo cha afya Chamwino, Dk. Zipora Mfugale amesema kuwa wamejipa kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo wa CHF iliyoboreshwa.