Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa amezungumzia tetesi na uvumi unaoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii, juu ya madai  ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kugombea  nafasi ya Ubunge wilayani humo .

Akizungumza na EATV & Radio Digital, Diwani huyo amesema kuwa tetesi hizo ni za uongo na kwamba zinatengenezwa na watu kwa maslahi yao binafsi.

''Mimi Makonda ni rafiki yangu toka 2000, hajawahi kuniambia hata siku moja anataka kugombea jimbo la Kigamboni, isipokuwa ni msaada mkubwa sana katika jimbo letu, ameweza kutupatia fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya Kigamboni'', amesema Diwani Dotto.

Aidha kwa mujibu wa Diwani Dotto, RC Makonda amewaahidi viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilayani humo kuwajengea ofisi ya ghorofa na kuwataka viongozi kujiamini na nafasi zao.