Kila mmoja ana mtizamo wake kuhusu harmonize kuondoka WCB baada ya kuvuna fadhila nyingi alizopewa na Diamond kama rais wa WCB pamoja na timu nzima.Kila mmoja yupo busy kumlaumu Harmonize kuhusu kuondoka wcb.wengine wakienda mbali na kusema atashuka kimziki.mara ndo mwisho wake..Nimeandika haya kuwakumbusha Watanzania sisi wasahaulifu ya kwamba "what goes around comes around "amini hivyo.

Diamond baada ya kuvuna fadhila za kutosha kwa Bob junior producer wake wa kwanza kumtoa . Wote tuliona namna ambavyo aliondoka kwa ugomvi..tena wa kutokusemeshana.
Watanzania hawa hawa wakasema mara atashuka kimziki mara mziki wake umefikia mwisho..kwani nyie mmekuwa manabii mpaka muwatabilie watu yajayo..

Diamond baada ya kuvuna fadhila alizopewa na meneja wake wa kwanza Papaa Misifa..aliondoka pale kwa ugomvi mpaka kudaina pesa. Diamond akaja kumlipa papaa baadaye akiwa na meneja mwingine

Diamond baada ya fadhila alizopewa na marehemu Ruge.kumuandalia shows,kumtangaza na mengine tuliona kilichotokea.mpaka anafariki Ruge,maelewano baina yao yalikuwa hamna.
Kuna na habari zisizokuwa rasmi kuwa hata Ali kiba aliwahi msaidia Diamond katika harakati za mziki. Vipi mawasiliano yao leo.

Kwa hiyo basi hapana jipya linalotokea WCB analolifanya harmonize. Ndo yale yale aliwahi kuyafanya Diamond kwa watu waliombeba na kumfadhili lakini alipopata alichokihitaji aliwaambia wanamdhulu,mara wanamnyonya,hawataki afike mbali.mwisho akaondoka na kwenda kunzisha maisha yake.jambo ambalo ni jema.

Suala la msanii kuachana na menejimenti yake hata kama ilimpa kila kitu .yeye akaenda kuanzisha maisha yake nje ya hiyo management sio Dhabi. Mbona hata America inafanyika tumemuona Lil Wayne alivyoachana na birdman. Kumbuka birdman kamlea Lil Wayne akiwa bado kinda mpaka anakuja kuwa msanii mkubwa. Walipopishana Lil Wayne akaondoka chini ya lebo ya Cash money.
Mwisho harmonize ni msanii mkubwa kwa sasa anahitaji nyumba yake na sio kuwa chini ya nyumba ya mtu. Jambo la kutoka WCB ni busara za juu na maamuzi magumu lakini yenye tija.Awekee bidii tu atafika. Anapopalenga