Msanii wa muziki nchini, Diamond Platnumz akanusha vikali madai ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake wa Bongo Flava, Lulu Diva.

Madai hayo yaliyoibuliwa na ukurasa maarufu wa udaku hapa nchini, yapelekea kumuibua Diamond na kukoment kwenye post hiyo huku akiwataka wamuheshimu kwa kila anaesambaza taarifa hizo.

Kupitia taarifa hiyo iliyotolewa na kukanushwa na mkali huyo hapa Instagram, ilieleza kuwa, "Yamezuka hayo baada ya video kusambaa ikiwaonesha wawili hao wakiwa katika mahaba mazito"

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa mkali huyo na matukio haya ya kuzushiwa, aliwahi pia kuzushiwa kutoka kimapenzi na mwanadada, aliyewahi kufahamika kuwa ni Video vixen Kimnana, ingawa hakuna aliyewahi kuthibitisha hilo.