Msanii wa muziki Diamond Platnumz amevutiwa na uwanja mkubwa wa kisasa wa mpira wa kikapu ‘Kigali Arena’ uliopo nchini Rwanda, Kwa kusema kuwa ametembea nchi zote hapa Afrika Mashariki lakini hajaona uwanja mkubwa kama huo.

Akiongea na Bongo5, Diamond Platnumz amesema kuwa anaiomba serikali ya Tanzania chini ya Rais Magufuli ijenge uwanja kama huo wa kisasa ili utumike kwenye michezo na matamasha mbalimbali ya muziki.

Akikazia maombi hayo, Diamond amesema kuwa endapo Serikali itampa uwanja anauwezo wa kujenga Arena yake kwani anaamini uwezo huo anao.

Uwanja wa Kigali Arena ulizinduliwa mwezi uliopita na Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame na utatumika kwa mchezo wa mpira wa kikapu pamoja na matamasha mbalimbali ya burudani.

Uwanja huo unauwezo wa kuchukua watu 10,000 kwa muda mmoja na una huduma zote muhimu ikiwemo Vyoo, Mabafu, Migahawa na viyoyozi pia vimefungwa.