DC Aagiza Watumishi Wanunue Ultra Sound ya Mil 30 Iliyoibwa
BAADA ya mashine ya Ultra Sound kuibiwa katika Hospitali ya Wilaya Bariadi mkoani Simiyu, Mkuu wa Wilaya hiyo, Festo Kiswaga, ameagiza watumishi wote 137 wa hospitali hiyo kuchangishwa fedha kulingana na kiwango cha mshahara ili kununua mashine mpya yenye thamani ya Tsh. Millioni 30.

“Ndani ya siku saba, hiyo Ultra Sound iwe imenunuliwa na ikabidhiwe kwangu.  Siku saba zikiisha mtu hajatoa hiyo fedha afukuzwe kazi.   Kama kuna mtu atahoji huko juu anihoji mimi na kama itaonekana nimefanya maamuzi yasiyofaa acha niende nyumbani,” amesema Kiswaga.

Aidha, amesema yupo tayari kufukuzwa kazi kwa kusimamia hili huku akimwagiza Ofisa Utumishi kumfukuza kazi mtumishi yeyote atakayekaidi agizo hilo ndani ya siku saba.