China imesema imeshtushwa na taarifa iliyopokea kutoka kwa bunge la Kenya kuwa kontena lililokuwa na vifaa vilivyotolewa kama msaada kutoka China na kuwasili siku ya Jumanne na kufunguliwa na maafisa wa bunge la Kenya lilikuwa tupu.

Taarifa nchni zinaashiria kuwa kontena hilo lenye vifaa vya msaada lilipelekwa katika makao ya bunge liliwasili likiwa halina kitu ndani.

Mtoto wa kiume wa Bin Laden ''amefariki''
Ofisi zapakwa kinyesi cha binadamu Burundi
Lissu ''tayari kuingia mahakama kuu ya Tanzania''
China imesema tukio hili ni la kwanza kuwahi kutokea ,na kwamba kwa miaka mingi imekuwa ikitoa misaada ya kirafiki kwa Kenya, ikiwemo vifaa tiba, vifaa vya ofisi, msaada wa chakula nakadhalika, na vyote vimekuwa vikiwasilishwa vikiwa salama kabisa.