Mtangazaji Casto Dickson ambae alishawahi kuwa kwenye mahusiano na Mwanadada Tunda amevunja ukimya na kumchana x wake huyo na mpenzi wake wa sasa ambae ni Mchekeshaji na mwigizaji Whozu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Casto amewataka Tunda na Whozu waache kutafuta kiki kupitia yeye na wasimuhusishe kabisa kwenye kiki zao.

“Msitafute kiki zenu kwa majina na jasho la waliotafuta wenzenu kwa jasho lao kwa upuuzi wenu. Kwako wewe X wangu na mpenzi wako tunaweza kutana mahakamani kwa sababu nazijua account zako fake zote! Nimechoka mnaitesa status yangu sio moyo wangu! Utumbo tu huo!” aliandika Casto lakini hata hivyo si Tunda wala Whozu walioibuka kujibu lolote.