AMEFUNGUKA! Mchumba mpya wa staa wa Bongo Muvi, Aunt Ezekiel, Alfo ameweka wazi kuwa hakuna mwanamke anayemzimikia kwenye hii dunia kama mwigizaji huyo.Kijana huyo raia wa Ivory Coast ambaye kapanda hewani, amesema Aunt ni kama dhahabu aliyokuwa akiitafuta kwenye nchi mbalimbali bila mafanikio hadi alipokutana naye Bongo.“Jamani ungejua ni kiasi gani ninampenda Aunt, ninamfananisha na dhahabu ambayo siku zote inang’aa haiharibiki hata kidogo, huyu ni mwanamke mzuri sana.“Dhahabu niliyokuwa ninaitafuta nchi mbalimbali nimeipata, kwa kweli nina amani moyo wangu umeanza kuwa na amani tofauti na huko nyuma, naweka wazi kabisa amenimaliza,” alisema Alfo na kusisitiza kuwa anatamani kuzaa na staa huyo watoto wawili.