Mastaa wa muziki nchini Kenya, Brown Mauzo na Otilie Brown wamewachanganya mashabiki ndani ya muda mfupi.

Hii ni baada ya mrembo @iam_amberay aliyedaiwa kutoka kimapenzi na Mauzo kuonekana kwenye Picha ya Pamoja na Otile.

Inadai kuwa Ambaeray na Otile wamekutana kikazi kwa mrembo huyo kutumika kama video vixen kwenye moja ya video za Otile Brown.

Brown Mauzo mapema leo, akatundika picha yake mpya mtandaoni akiwa na mrembo mwingine sambamba na maelezo ya kuwa ‘Mr Love Man”.