Msanii na mtayarishaji wa muziki Bob Junior, amejisifia kuwa amebarikiwa nguvu za kiume tofauti na wanaume wengine.


Msanii huyo amezungumza hayo kupitia eNewz ya EATV, akijibu tuhuma za kuingiza wanawake na kufanya nao mapenzi studio kwake.

"Kawaida tu mimi ni rijali, ukikuta mwanamke ana mahaba na mimi nampa tu nguvu za kiume ambazo nimejaaliwa na M/Mungu napaswa niwape watoto wa kike ambao wanahitaji mapenzi kutoka kwangu, ukiwa na nguvu za kiume ni baraka tosha kuna watu wanazitafuta hizo".

Aidha Bob Junior ameendelea kusema kuwa hawachukui wanawake wa watu ila wao wenyewe ndio wanamtafuta, wanampenda na anataka hata akifa aache kizazicha watoto 20 au 30.

Pia amezungumzia bifu kati ya Mr Blue na Bonge La Nyau, ambapo amesema hawezi kuingilia kati kwa sababu wote hao ni ndugu zake ila yupo tayari kuwapa "Beat" bure ili wafanye kazi kwa pamoja.