Binadamu afunga ndoa na Mbwa
Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Elizabeth Hoad raia wa Uingereza,  amefunga ndoa na Mbwa wake aitwaye Logan katika kipindi cha Television Nchini humo.


Baada ya kufunga ndoa, Mwanamke huyo ameeleza aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Wanaume 221, kati ya hao Wanne ndio walimvalisha pete ya uchumba lakini imeshindikana kuolewa.

Pia mwanamke huyo amesema ameamua kufunga ndoa na Mbwa wake "Logan", kwa sababu ya kuchoshwa na Tabia za Wanaume wazee kupenda Wanawake wadogo na Wanawake wadogo kupenda Wanaume wazee.

Aidha Elizabeth ameendelea kusema Mbwa huyo ana maana kubwa sana kwake kwa sababu wameshasaidiana kwa vitu vingi hasa wakati alipoumizwa na Wanaume ambao aliwahi kuwa nao, pia ana marafiki zake 10 ambao wameamua kufunga ndoa na Mbwa wao.

Akiweka kiapo katika sherehe ya kufunga ndoa hiyo Elizabeth aliahidi kuwa, "kwa mwili wake wote atatembea na Mbwa Logan, atamjali na kumpenda siku zote za maisha yake na kulala nae kitanda kimoja" amesema Elizabeth.