Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi kombe na cheti Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Bernard Kibesse (kulia) baada ya Benki Kuu kuibuka mshindi wa Kwanza kundi la Sekta ya Fedha, katika Maonesho ya Nane Nane 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mmkoani Simiyu Agosti 8, 2019.(Picha na K-VIS BLOG/Khalfan Said).
Dkt. Kibesse akinyanyua juu kombe na cheti baada ya kukabidhiwa na Waziri Mkuu.(Picha na K-VIS BLOG/Khalfan Said).
Meneja wa Uhusiano wa Umma na Itifaki, Benki Kuu ya Tanzania Bi. Zalia Mbeo, akinyanyua juu kombe na cheti ambavyo BoT ilishinda katika Maonesho ya Nane Nane 2019 yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwa nja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Agosti 8, 2019. (Picha na K-VIS BLOG/Khalfan Said).
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), akimsikiliza Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Bernard Kibesse, wakati akifafanua baadhi ya mambo, wakati Mhe. Majaliwa alipotembelea banda la BoT kwenye kilele cha Sherehe za Maonesho ya Nane Nane viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Agosti 8, 2019. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima. (Picha na Innocent Mmari-BoT).
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akifafanua jambo kwenye banda la BoT alipotembelea banda hilo viwanja vya Nyakabindi.((Picha na Innocent Mmari-BoT).
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia katika kilele cha Sherehe za Nane Nane zilizokwenda sambamba na ufungaji wa maonesho ya Nane Nane Kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu Agosti 8, 2019. (Picha na K-VIS BLOG/Khalfan Said).
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally (wakwanza kushoto), Waziri wa Mifugo ya Uvuvi, Me. Luhaga Mpina, (wkawanza kulia), Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (waili kulia) na Mkuu w aMkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (wapili kushoto), wakipiga makofi baada ya kuimbwa wimbo wa Taifa mwanzoni mwa sherehe za kilele cha Nane Nane Mkoani Simiyu. (Picha na K-VIS BLOG/Khalfan Said).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pamba wakati alipotembelea Chama cha Ushirika cha msingi cha Itemelo, eneo la Dutwa mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally, Wa nne kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa tano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Japhet Hasunga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaidiana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wa nne kulia) kupandisha pamba kwenye mzani wa kielektroniki wakati alipokaguaununuzi wa pamba kwenye Chama cha Ushirika cha Msingi cha Itemelo, eneo la Dutwa mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akipunga mmkono wakati akiondoka viwanja vya Nyakabindi.(Picha na K-VIS BLOG/Khalfan Said)
Dkt. Kibesse akiwa amekamata vikombe katika picha ya pamoja na watumishi wa BoT mbele ya banda la Benki hiyo viwanja vya Nyakabindi. (Picha na Innocent Mmari wa BoT).

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu.

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT), imeibuka Mshindi wa Kwanza kwa taasisi za Fedha na Mshindi wa Pili wa Jumla (Second Overall Winner) katika Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Nyakabindi, nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Kutokana na ushindi huo, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, alimkabidhi vikombe vyote viwili na vyeti, Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Bernard Kibesse, katika sherehe za kilele cha Nane Nane Agosti 8, 2019.

BoT, ilishiriki Maonesho hayo yaliyoanza Agosti 1, 2019 ili kuwaelimisha wananchi majukumu ya benki hiyo wanayotekeleza kila siku lakini pia kuishauri Serikali kufanya utafiti na kutekeleza Sera ya Fedha inayolenga zaidi kuhakikisha kunakuwa na Mfumuko mdogo wa bei.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameipongeza BoT kwa juhudi zake za kuisaidia Serikali kuweka njia nzuri kuwawezesha wanunuzi wa pamba ili kununua pamba yote.

Lakini pia Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza Benki hiyo ambayo ndiyo msimamizi wa shughuli za kifedha hapa nchini kutokana na kuweka usimamizi mzuri wa uingiaji wa fedha za kigeni ambao sasa unaendana na muelekeo wa uchumi wa nchi.