Mkali wa muziki wa RnB Bongo Ben Pol, amejibu kuhusu issue ya kushindana na msanii Ommy Dimpoz kula bata nchi za nje pamoja na tuhuma za kwamba anafanya kazi yake ya usanii kivivu.

"Mimi ni mtu ambaye nafanya kazi, naipenda kazi yangu sio mvivu na nimeshawatumikia sana watanzania na mashabiki zangu, kwahiyo kama mfanyakazi na watu wanaona bidii zangu sio mbaya siku mojamoja kula raha ni mambo ya kheri tu".

Pia Ben Pol ameeleza zaidi kuhusu tetesi za ushindani kati yake na Ommy Dimpoz, kwa kusema hakuna ushindani wa kula bata kati yao bali huwa wanapishana tu na kila mtu anakwenda na safari zake.

Ben Pol amekuwa msanii ambaye anakula sana bata siku za hivi karibuni katika sehemu mbalimbali kama Dubai, Marekani na kwingineko haswa baada ya kuwa na mahusiano na mchumba wake Anerlisa Muigai, ambaye ni raia wa Kenya