Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida, Salum Mahami (kulia), akiongoza kuomba dua katika Swala ya Eid Al-Haji iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye mkoani hapa leo. Kushoto  ni Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Singida, Burhan Mlau.
 Sheikh Shabani Mkanga akisoma hutuba katika swala hiyo.
 Waumini wa dini ya kiislamu wa mkoa wa Singida wakishiriki swala hiyo.
 Waumini wa dini ya kiislamu wa mkoa wa Singida wakishiriki swala hiyo.
 Wanawake wa Kiislamu wakiwa kwenye swala hiyo.
 Watoto na wakishiriki na wazazi wao katika swala hiyo.
 Dua ikifanyika.
swala ya Eid -Al- Haji baada ya kumalizika

Na Dotto Mwaibale, Singida

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata)  Mkoa wa Singida limetoa pole kwa Rais Dkt.John Magufuli kufuatia msiba wa watu 71 waliofariki kwa ajali ya kuungua moto mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.

Pole hiyo kwa Rais imetolewa na Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Burhan Mlau katika swala ya Eid- Al-Haji iliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye mkoani hapa.

"Tunampa pole Rais wetu kwa msiba huu mkubwa tulioupata pamoja na wafiwa na tunawaombea majeruhi wote wapate nafuu waweze kurejea katika shughuli za ujenzi wa taifa" alisema Mlau.

Mbali ya Rais Magufuli wengine waliopewa  
pole hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe pamoja na wananchi wote wa mkoa huo na kuwa Taifa limepoteza nguvu kazi kubwa.

Katika swala hiyo Mlau aliwataka Waislamu wa mkoa huo kuwa kitu kimoja na kuondoa utengano kupitia taasisi zao mbalimbali badala ya kutengana.

"Nawaombeni ndugu zangu waislamu tuendelee kushikamana na kupendana kupitia taasisi zetu jambo ambalo litadumisha uislam wetu na kumpendeza mwenyezi mungu" alisisitiza Mlau.

Katika kusherehekea sikukuu hiyo Mlau aliwaomba waislam wa mkoa huo kusherehekea kwa utulivu  na amani huku wakiwangalia watoto wao kwa ukaribu.