BAADA ya kimya cha muda mrefu, msanii wa filamu za Kibongo ambaye pia amewahi kuwa mtangazaji wa runinga, Lulu Semagongo ameibuka na kueleza sababu za kupotea kwake.Akistorisha na Shusha Pumzi, Aunty Lulu alisema kuwa sababu iliyompoteza kwenye ulimwengu wa sanaa ni mapenzi kwani mpenzi wake aliyenaye ana wivu sana na hataki aonekane kwenye filamu wala vyombo vya habari jambo ambalo limemrudisha sana nyuma.

“Nipo tu nafanya biashara ikiwa ni baada ya kupigwa stop na mpenzi wangu nisiendelee na sanaa kisa wivu wake lakini ipo siku nitarudi kwenye gemu kwa kasi kama ni kuachana tuachane tu maana hata kazi yangu ya utangazaji hataki niirudie wakati bado ninaipenda,” alisema Aunty Lulu.