Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo amefanikiwa kutetea tena nafasi yake ambapo ataliongoza Kanisa hilo kwa kipindi kingine cha miaka 4 ijayo kufuatia uchaguzi uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika eneo la Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Makumira kilichopo Usariva nje kidogo ya Jiji la Arusha.Askofu Dkt. Shoo ameshinda kwa kura 148 dhidi ya kura 78 za Askofu Abernego Keshomshahara wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Uchaguzi huo ilibidi usubiri hadi majira ya saa nane za usiku wa kuamkia leo kabla ya Askofu Dkt. Shoo kutangazwa mshindi kutokana na kupitia michakato kadhaa ya vikao vya Maskofu wenyewe, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kanisa hilo na baadaye Mkutano Mkuu wa kumchagua Mkuu wa KKKT Tanzania.

Baada ya kuchaguliwa Askofu Dkt. Shoo amehimiza umoja na ushirikiano katika kuliimarisha kanisa huku akitolea mifano ya vifungu mbalimbali vya Biblia ikiwa ni sehemu ya kukazia mwito wake kwa watu anaowaongoza