Baada ya kuripotiwa kuwa mwigizaji Angelina Jolie na aliyekua mume wake Brad Pitt kupeana talaka rasmi April 12,2019 na kuripotiwa kuwa walipewa nafasi ya makubaliano kuhusiana na mali ikiwemo na malezi ya watoto wao 6.

Sasa kwenye mahojiano na kipindi cha ‘Entertainment Today’  Angelina Jolie ametaja sababu ya kuachana na mume wake Brad Pitt baada ya mashabiki wengi kuhoji na kutaka kujua sababu ya wawili hao kuachana, Angelina alieleza kuwa kikubwa ni kuwa Brad alifikia wakati ambao alikua akilewa sana na kushahau majukumu yake kama mume na baba katika familia yenye watoto sita.

Angelina Jolie aliendelea kueleza kutokana na tabia yake ya ulevi alikuwa akipoteza nafasi nyingi kwenye filamu za Holly Wood pia mwigizaji huyo ambaye kwa sasa ana miliki tovuti ya kupunguza mwili (Keto Original Diet) aliweka wazi kuwa Brad alipata wivu kuhusu tovuti hiyo na kuhisi kuwa asingepata nafasi ya kuitangaza kwa sababu ilihusisha wanawake tu.

Fahamu kuwa Brad Pitt na Angelina Jolie walifunga ndoa mwaka 2014 na kubahatika kupata familia yenye watoto 6 pia wameshiriki kwenye filamu nyingi pamoja ikiwemo Mr & Mrs Smith, By The Sea ambazo ziliwapatia umaarufu mkubwa duniani.