BAADA ya habari kutapakaa kama moto wa kifuu akikiri kuokolewa na msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ baada ya kumlipa hela shoo na kulipa kodi, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amewamaindi watu mitandaoni wanaomsema vibaya kuhusu hilo.
Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Amber Lulu alisema kuwa yeye siyo wa kufeki maisha hata siku moja na ni kweli alikuwa hana kodi na hela aliyompa ilimsitiri sana mbali na kulipia kodi. “Eti utakuta mtu anasema huna aibu kusema nilikuwa sina kodi kwa kumuogopa nani sasa na kwa nini maana amenipa kazi na nimefanya akanilipa shida iko wapi na nani anaumia sasa?” alimaindi Amber Lulu.