Wasanii Alikiba na Aslay wamewaacha katika mtihani mashabiki zao, baada ya kuonesha kama wana ujio wa kazi mpya kati yao.

Aslay amewachokoza mashabiki wa muziki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya kuweka picha akiwa studio na Alikiba pamoja na wasanii wengine wa Kings Music.

Eti Tuanze AUDIO au VIDEO????

Ameandika, ''Eti tuanze na Audio au Video'', jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa 'coments' mbalimbali wengine wakitaka aachie vyote Video na Audio.

Lakini bado haijajulikana kama Aslay amefanya ngoma na Alikiba au wasanii wa Kings Music. Tumemtafuta kuzungumzia hilo lakini simu yake na ya meneja wake Chambuso zote hazipokelewi.