Ajibu Atangaza Rekodi Mpya Simba
IBRAHIM Ajibu, Kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa msimu ujao anataka kuweka rekodi mpya tofauti naile aliyoiweka miaka miwili alipokuwa ndani ya Simba.


Ajibu kwa sasa anasumbuliwa na goti yupo Bongo kwa ajili ya matibabu huku hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza na UD do Songo ya Msumbiji.


Akizungumza na Spoti Xtra, Ajibu alisema kuwa kwa sasa anajipanga kufanya vizuri msimu ujao kwa ajili ya mashabiki na timu ya Simba.

“Ninaamini bado nina nafasi ya kufanya vizuri na kuweka rekodi mpya ndani ya Simba tofauti na wakati uliopita, hivyo mashabiki waendelee kutupa
sapoti,” alisema Ajibu.

Ajibu amecheza ndani ya Simba kwa muda wa misimu mitatu ambapo ilikuwa msimu wa 2014/15, 2015/16 na msimu wa 2016/17 alipachika jumla ya mabao 23 amerejea tena msimu wa 2018/19 akitokea Yanga.