Obadele Kambon, Mmarekani mwenye asili ya kiafrika hajawahi kujutia hatua yake ya kuhamia nchini Ghana tangu mwaka 2008. Aliapa kutorejea tena nchini humo baada ya tukio la kukamatwa kwake analoamini lilichochewa na ubaguzi wa rangi. Bw Kambon ambaye sasa ameanza upya maisha katika taifa ambalo lilikuwa kitovu cha biashara ya utumwa anasema kuwa anafurahia uhuru aliokosa nchini Marekani alikozaliwa.Anasema hana hofu ya kukamatwa na polisi au cha kuogofya zaidi kuuawa kwa mwanawe wa kiume. Hiyo ni hali iliyomkumba Tamara Rice aliyekuwa na miaka 12 ambaye aliuawa katika bustani ya Cleveland, Ohio, mwaka 2014 akiwa anacheza na bunduki badia ambayo polisi walidhani ya kweli.

Kukamatwa kimakosa
Kifo cha mvulana huyo mdogo kilisababisha maandamano makubwa mjini Cleveland, na kuwa mwanzo wa vugu vugu la kupigania uhuru wa tu weusi maarufu ”Black Lives Matter”.

Bw. Kambon anasema mwamko mpya maishani mwake ulikuwa mwaka 2007 alipokamatwa na kushtakiwa mjini Chicago – alipokuwa anaishi – baada ya kutuhumi wa na maafisa wa polisi kwa kuweka bunduki chini ya kiti cha gari lake kwa lengo la kuitumia kuwajeruhi watu. Anakumbuka kesi hiyo hicho kwa mshtuko mkubwa na wakati wa kusikizwa kwa kesi dhidi yake, aliapa: “Kutokaribia maeneo yanayolindwa na maafisa wa polisi wazungu asije akafungwa na kutenganishwa na familia, mke na mtoto wake kufumba macho na kufumbua.”

Bw Kambon – ambaye ali dola 30,000 (£24,000) na kuhamia mji mkuu wa Ghana, Accra, mwaka uliofuata. Mke wake, Kala aliungana nae na wanandoa hao wana watoto watatu- Ama, Kwaku na Akosua.

Mtalii akipiga selfie katika kasri la Cape Coast Augosti 18, 2019
Kasri la watumwa katika pwani ya Ghana sasa ni kivutio kikubw acha watalii
Bw. Kambon alianza kusomea shahada ya uzamifu ya lugha katika Chuo Kikuu cha Ghana mwaka 2009 na sasa anafunza katika chuo cha elimu ya Kiafrika.
Tangu alipohamia Ghana, amegundua hajihisi kuwa mhanga wa ubaguzi wa rangi wala kutukanwa kutokana na rangi ya ngozi yake.

Anaelezea kuwa marafiki zake pia walijihisi hivyo walipohama Marekani.

Kambon sasa anaweza kuzungumza lugha mbili za Afrika Magharibi- Akan na Yoruba – anajaribu pia kuzungumza kidogo lugha ya Wolof.

Amekuwa akijifunza kusoma na kuandika Kiswahili ambayo ni lugha kuu katika eneo la Afrika Mashariki na pia inazungumzwa katika badhi ya sehemu za Kati na Kusini mwa Afrika.

Men removing the Gandhi statue
Obadele Kambon aliongoza kampeini ya kuondolewa kwa sanamu ya Mahatma Gandhi. katika Chuo Kikuu cha Ghana.
Amekuwa pia akijaribu kuanganzia masuala historia ya ukoloni kwa njia zingine. Mwaka 2018, alifanikiwa kuongoza kampeini ya kuishinikiza Chuo Kikuu cha Ghana kuondoa sanamu ya kiongozi wa uhuruwa India Mahatma Gandhi. Alisema ni bora kuweka sanamu ya kutambua mashujaa wa Kiafrika badala ya mtu ambaye aliwahi kutumia lugha ya ubaguzi dhidi ya raia wa Afrika Kusini- na alisema kuwa Wahindi walikuwa “bora kabisa” kwa watu weusi.

“Tukionesha kuwa hatujiheshimu au kudharau mashujaa wetu basi tutakuwa na tatizo ,”Bw. Kambon. Japo utumwa ulifanyika kabla ya mwaka 1619, mwaka huo ulitajwa kuwa wa makumbusho ya miaka 400 tangu watumwa kwa kwanza wa kiafrika waliwasili nchini Marekani. Makasri ya watumwa ya Elmina na Cape Coast katika pwani ya Ghana yalikuwa vituo vikubwa vya biashara ya watumwa ambapo amamilioni ya waafrika walitekwa na kuingizwa kwenye meli na kusafirishwa na hawakuwahi kurudi tena makwao.