Msichana mwenye umri wa miaka 23, Alexa Terrazas wa nchini Mexico, ameanguka futi 80 kutoka ghorofani pindi alipokuwa akifanya mazoezi ya Yoga.


Alidondoka kutoka ghorofa ya tano na kuangukia katika eneo la kuegesha magari kwenye ghorofa hilo, Jumamosi iliyopita alilokuwa akifanyia mazoezi lakini alipona baada ya kukimbizwa hospitali.

Picha ya msichana huyo kabla hajadondoka kutoka ghorofani ilisambaa katika mitandao ya kijamii, akionekana amejining'iniza kichwa chini miguu juu kwenye uzio wa chuma.

Inaelezwa kuwa alianguka majira ya saa 1:10 Usiku, ambapo alikimbizwa katika hospitali ya karibu na kufanyiwa upasuaji kwa saa 11, kutokana na kukutwa na nyufa katika miguu yake, mikono, kichwani na mapajani.